Karibu rafiki yangu kwenye makala yetu ya leo.
Leo tunaenda kuangalia kwanini tunapitia kwenye nyakati ngumu.Nyakati ngumu zimekuwa ndiyo mwalimu mkuu kwetu.
Pale unapopitia nyakati ngumu zinakufanya ufanye maandalizi ya kubeba majukumu yako yatakayokuwezesha kufikia mafanikio yako
Watu huwa hawajali sana kile unachokisema,bali hujali kile unachokifanya.Hakuna mtu anayetaka kuwa masikini,hakuna anayetaka kuteseka.
Kila mmoja wetu anayo nia ya dhati ya kupambana ili kuyafikia malengo yake. Hivyo inapotokea ukakwama jua ni mojawapo ya mambo yaliyopo kwenye safari yako.
Kumbuka mshale unaweza kufyatuka pale unapovutwa kwenda nyuma.Pale unapoona maisha yakikurudisha nyuma na kupitia magumu jua yanakwenda kukupatia kitu kikubwa huko mbele.Hivyo ongeza nguvu na endelea kupambana.
Jisamehe kwa maamuzi mabaya uliyoyafanya.Jisamehe kwa makosa yako uliyoyafanya.Jua kinachotakiwa ni wewe kusonga mbele huku ukiwa umeshajua nini kilikufanya ukaanguka mwanzo.
Unapaswa kuachana na vitu vyote ambavyo huwezi kuvidhibiti.Kama umepata hasara kubaliana nayo.Hivyo jiimarishe ondoa wasiwasi,futa aibu.Jijali na uwajali wale wote walio na umuhimu kwako.
Pambana kuifikia ndoto yako,na hakikisha unajipenda kwanza wewe, vinginevyo hakuna anayeweza kufanya hivyo kwa niaba yako.
Pale utakapofanya vitu vyako vizuri utawavutia watu ambao watataka kuwa na wewe.Na pale utakapozungukwa na watu sahihi ndipo utakapoanza kuyaona mafanikio yako.
Kumbuka Ndoto zako zitaendendelea kutimia kwa wewe kuendelea kukuza biashara yako,na kuanzisha biashara nyingine mpya.
Hivyo endelea na mapambano fanya kazi kwa bidii na maarifa.Weka nidhamu kwenye kazi yako na utakapogundua pochi yako utaiona faida ya uwekezaji wako.
Maisha mazuri ni fursa kwa wale wote waliotayari kuyapambania,na siyo wale wanaokaa na kuwaangalia wengine . Usiogope ukaipoteza fursa ya wewe kuwa na maisha mazuri ya Ndoto yako.
Usiache kujaribu maana kila mafanikio huanza na wazo la kutaka kujaribu.ujinga na woga huharibu fursa nyingi.hujachelewa anza leo kufanya kile unachokitaka
Mwandishi wa makala hii ni Emanuel mcharo.wasiliana naye kwa barua pepe mcharoima@gmail.com.